Labels

Monday, June 25, 2012

happy blue monday!


Wasaalam wadau wa blog.

Karibuni tena katika blog yetu tukianza wiki ya mwisho ya mwezi wa sita mwaka huu wa 2012.

Pole nyingi kwa wapenzi wakubwa wa timu ya Uingereza kwa kutolewa katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa ya Ulaya, Poleni wapenzi wa Barbz wa jumba la kaka mkubwa aliyekuwa akiwakilisha bondeni kwani naye "out" toka mjengoni!

Poleni kwa Tanzania na wazalendo wenzangu kwa hofu na mashaka mengi yaliyotawala kwa vitisho na migomo ya wataalamu wetu wa tiba, madaktari!

Tena poleni zaidi ndugu zetu wa Kenya kwa milipuko na mashaka yanayoendelea kuwatawala.

Basi baada ya msururu wa pole zote hizo nawaaahidi kuendelea kuwakilisha na kuelimisha zaidi kwa mada nyingine nyeti hasa baada ya kuwaletea tafsiri ya mada za wiki iliyopita katika lugha yetu ya kibantu ili kuweza kuwanufaisha na wale ambao ni wapenzi zaidi wa lugha ya taifa!

Happy productive week ahead of everyone!

No comments:

Post a Comment