Mahusiano ni kama mchanga uliowekwa katika kiganja cha mkono wako, utakapoushika vizuri na wazi, mchanga huo utabakia kuwa katika kiganja. Pale utakapojaribu kufunga mkono, kuminya na kubana kwa nguvu mkono wako ili kuuzuia mchanga huo, basi bila shaka utaanza kupenya katikati ya vidole vyako na kumwagika chini. Utaweza kuuzuia kiasi utakapoanza kumwagika, lakini mwingi utaishia chini. Mahusiano ndivyo yalivyo.
Mahusiano mengi ambayo yanashindikana na hatimaye kuelekea
kuvunjika, talaka na kuachana hutokana na sababu kubwa ni : baada ya muda
fulani katika mahusiano, mawasiliano yanapungua baina ya wawili hao,
kutokuelewana kunajitokeza na maelewano katika mambo ya msingi yanatoweka!
Sababu nyingine kubwa ambayo inapelekea kuvunjika kwa
mahusiano ni kutopeana muda wa kutosha kuwa pamoja kama wapenzi, katika dunia
ya leo yenye changamoto nyingi kujitolea muda kuwa pamoja na mwenzako, familia
ama ndugu imekuwa ni tatizo kubwa.
Tatizo kubwa zaidi katika mahusiano linakuja hasa kutokana
na sababu watu wengi wanajiingiza katika mahusiano ili kupata kitu
fulani: wanajaribu kupata mtu ambaye atawafanya wajisikie vizuri.
Ukweli ni
kwamba , namna pekee ambayo unaweza kupangilia mahusiano yako yaweze kudumu na
kushamiri ni kuwa tayari kujitolea zaidi kuliko kutegemea kuwa mpokeaji tu katika mahusiano yenu!
Talaka na kutengana katika mahusiano huacha madhara makubwa
sana kwa wahusika hasa kwa upande wa afya zao; usumbufu wa akili hutokea, na
matatizo kama midhaiko na ukosefu wa amani. Kumukumbu za mahusiano yaliyopita
hukuandama na kusababisha kujishushia heshima, kutokujiamini na mambo mengine
kama hayo.
Ni vigumu sana kupita katika matatizo kama hayo na kuweza
kuhimili hali kama hizi baada ya kutokea. Hutokea hali ya kutojiamini tena na
kuogopa kuingia katika mahusiano mengine ama kukurupuka na kujiingiza katika
mahusiano mbalimbali bila kutafakari. Mara nyingi uwezo wa kufikiri na hata wa
kufanya kazi wa watu waliokumbwa na matatizo kama haya hupungua, na hubadilika
toka kuwa yenye kujenga zaidi na kuwa ya kubomoa zaidi kwa maisha binafsi ya
wahusika. Madhara haya hutokea katika mazingira amabayo muhusika anapambana kujiweka katika hali ambayo atajisikia kila kitu kiko sawa kwa upande wake, wakati inakuwa sivyo.
Jambo ambalo linasababisha UELEWA/ MAELEWANO kuwa jambo gumu
zaidi ni kuwa yatupasa zaidi kusikiliza na kuelewa nafasi ya upande wa
pili wa wenzetu ambao tuna mitazamo tofauti. Hatupaswi kukubaliana nao, lakini
hatuna budi kuwasikiliza. Labda, kutokana na ustaarabu yanaweza kutokea maelewano
ya pamoja namna gani kila mmoja ameelewa namna mwenzake anavyochukulia na kuamini katika
jambo husika… hata kama mwisho wa siku mtakuwa hamkubaliani kati yenu bado.
Hivyo, kabla hujakumbwa na bahati mbaya ya kujiingiza katika
mahusiano yatakayoishia kuvunjika ama talaka, chukua tahadhari kumwelewa na
kuelewana na mpenzi wako vizuri zaidi, ni vyema kila mmoja akajua uwezo na
udhaifu wa mwenzi wake na namna gani anaweza kukabiliana na mapungufu
yatakayojitokeza.
Ijumaa Karim...
No comments:
Post a Comment