Labels

Thursday, April 16, 2015

Kuvunjika kwa Penzi?!


 
KWANINI WATU HUACHANA KATIKA MAPENZI?

Wakati watu wanapoingia kwenye mapenzi, hufanya hivyo kwa sababu mbalimbali. Baadhi ya watu ni kwa sababu ya upweke, na wamekuwa wakihitaji kukutana na mtu ambaye wanaweza kuzungumza naye na kujumuika naye kwa kipindi fulani kwa namna ya undani. Ingawa wanaweza kuwa na marafiki, wanajiona maisha yao hayajakamilika mpaka watakapokutana na watu fulani. Na pindi wanapokutana na watu hao, wanagundua kuwa kwa hakika hawakumhitaji mtu huyo. Wanagundua kuwa wanaweza kusimama wenyewe. Walichokuwa wanakitafuta, tayari wanacho. Kamwe huwa hawagundui hilo. Hivyo, wako ambao wameingia kwenye mapenzi kwa sababu isiyo sahihi na pindi sababu hiyo inapotimizwa, wanajiondoa kwenye mapenzi.

Ni rahisi sana siku hizi kuingia kwenye tamaa na kukosea kwa kudhani kwamba uko kwenye mapenzi. Na pindi tamaa hiyo inapokwisha, unajiondoa kwenye mapenzi.

Watu wengi wanaojiingiza kwenye mapenzi kwa sababu ya mihemko na siyo dhati ya moyo, ndio wale wanaoishia kuwa na wapenzi wengi katika vipindi mbalimbali. Pindi mihemko inapokwisha, wanajitoa mapenzini na kwenda kwa mtu mwingine ambaye ana mihemko naye.

Mihemko ni matarajio ya mapenzi. Haiwezi kudumu milele. Unapokutana na mtu mpya, kunakuwa na kutokea kwa kichocheo mwilini, hasa kama kuna vitu mnavyofanana. Mwili wako hujibainisha na mtu huyo na mara moja hujiskia vizuri kuwa na mtu huyo. Hamu yako ya kutaka kufanya mapenzi naye hutokea na hili huendelea kwa usiku mzima au kwa usiku mwingine mwingi kutegemea na jinsi utakavyojiridhisha.

Kutoka na mtu fulani bila ya kufanya mapenzi husababisha uhusiano kukomaa kwa sababu hudumisha mihemko. Mwili wakati wote hupata misukumo na haitulizwi kikamilifu hivyo kuendelea kuwa na matamanio. Matarajio hayo ya mapenzi huendelea kuwa makubwa na hivyo kuwa na mihemko mikubwa. Lakini pindi unapofanya mapenzi hupunguza mihemko yako wakati huo. Kila wakati unapofanya mapenzi mihemko yako hupunguzwa na hamu ya mapenzi huendelea kupungua.

Wakati wote huanza kwa kuwa juu zaidi na zaidi unapoanza kufanya mapenzi na mtu matarajio yako huwa juu, baada ya hapo huanza kupungua zaidi na zaidi kwa vile kufanya mapenzi huchukua nguvu zako nyingi. Uhusiano ulioegemea kwenye ngono hudumu kwa muda mfupi kuliko uhusiano usio wa kingono.

Sababu nyingine inayowafanya watu kuondoka kwenye mapenzi ni kwa sababu ya kutofikiwa kwa matarajio yao. Wanapokuwa kwenye mapenzi, wanakuwa na matarajio makubwa, kutegemea na kile wanachokitaka. Lakini baada ya muda fulani wa uhusiano wanagundua kuwa matarajio yao hayakufikiwa. Labda walitaka mtu ambaye atawasifia na kuwakubali, lakini hili linaweza lisijitokeze. Badala yake wanakuwa na mtu ambaye anawaita majina na kutowaheshimu. Baada ya kutosheka, hujitoa mapenzini na mtu huyo na kwenda kwenye uhusiano mwingine na mtu mwingine ambaye hukidhi mahitaji yao.

Watu wengi husukumwa mapenzini na familia zao. Utaona wamekuwa wakiulizwa wakati wote na marafiki zao: ‘utaoa au kuolewa lini?’ ‘Una rafiki wa kiume/kike?’ Au: ‘mtazame kijana yule mzuri’, ‘wenza wale wanapendeza’. Au kwa kwa kuamsha wivu: ‘ John anajua mapenzi, amenitumia maua kazini’. Au kwa kukumbusha siku ya kalenda: ‘Tarehe 14 Februari ni Siku ya Wapendanao’. Au kwa kutaja filamu za mapenzi: ‘How Sally met Harry’. Au kwa kusimulia simulizi za kuvutia: ‘Cinderella, Sleeping Beuty, Snow White’. Hadithi hizi zote ni za wasichana waliotaka kuokolewa na mwana wa mfalme na kuanguka kwenye mapenzi makubwa naye.

Hivyo kuna misukumo kwa wanaume na wanawake kujiingiza kwenye mapenzi.

Sababu nyingine inayofanya watu kujitoa mapenzini ni kutohudumiwa na wapenzi wao. Wanapokutana na mtu kwa mara ya kwanza huwa mzuri, anayependeza na mwema. Lakini baada ya muda fulani hubadilika na kuwa wenye lugha mbaya. Ama huwapiga au kuwatukana. Mtu hawezi kuvumilia zaidi mambo haya na hivyo hujiondoa mapenzini na kuendelea na maisha yao na kutafuta mtu mwingine atakayemhudumia vizuri. Hakuna mtu aliye tayari kutendewa vibaya ingawa baadhi ya watu huvumilia kwa muda fulani. Lakini kuvumilia huko hakumaanishi kuwa wanafurahia.

Wavulana hasa, hujifanya kuwa wazuri mwanzoni na baadaye hubadilika. Wavulana wanaofanya hivyo huwa wanajielewa lakini hujifanya kuwa wazuri wanapokutana na wanawake na wakati wanawake wanapokuwa karibu nao, ukweli wao hudhihirika, Kwani hawataweza kujifanya tena.

Hata hivyo si wavulana wote wana tabia hiyo. Kwa hakika wavulana walio wengi ni wazuri wakati wote. Bado watu huwa rahisi kutambulika wanapojifanya kama watu wazuri. Hivyo kama unamjua mpenzi wa zamani wa mtu utamwelewa vizuri mtu huyo. Hata kama mtu atajifanya kuwa mzuri, wakati wote huwa kuna dalili chache ambazo zitakuwezesha kujua ukweli halisi japo wengi hili hulidharau. Hulidharau hadi linapojitokeza. Kisha hubaki kushangaa kilichotokea. Kilichotokea ni kuwa ulidharau mabaya na kukumbatia mazuri. Na hilo limefanya mabaya kukua zaidi na zaidi mpaka kufikia mtu kutoweza kuyazuia tena na hivyo kuvunjika moyo au kujiondoa mapenzini na kuilalamika dunia. Dunia ni nzuri kwa wote wanaofanya uungwana . Huwezi kudharau mabaya na kukumbatia mazuri.

Na mwisho japo si kwa umuhimu kwa nini watu hujitoa mapenzini ni kwa vile hawakuwa kwenye mapenzi tangu mwanzo. Hakukuwa na hali ya udhati wa moyo; lilikuwa ni wazo tu. Wazo la kuwa kwenye mapenzi hujitokeza lakini huwa vigumu kubaki mapenzini. Unapaswa kuendelea kufanya mazuri. Unapaswa kuendelea kumkubali mpenzi wako. Lazima uendelee kumsaidia mpenzi wako. Lazima uendelee kumsaidia mpenzi wako hata katika vipindi vigumu, lazima ujitoe na kuwa pamoja naye kutatua matatizo kwa pamoja na kufurahia ushindi kwa pamoja.

Kuwa kwenye mapenzi na mtu hutangazwa sana kiasi kuwa watu wengi kujiingiza bila ya kuelewa kwa kina kile wanachokifanya. Hawajui hasa maana halisi ya kuwa kwenye mapenzi. Wanafikiri ni kama duka la bidhaa ambapo mtu huenda wakati kuna bidhaa na kutokwenda wakati hakuna bidhaa. Unapokuwa kwenye mapenzi unapaswa kwenda kunapokuwa na bidhaa (mhemko) na hata wakati hakuna bidhaa (mhemko) utabaki kuwa pale mpaka bidhaa zitakapokuja tena (mhemko).

Mihemko haidumu milele lakini kuwa katika mapenzi hudumu. Mihemko inachangia uhusiano kuwa wa kusisimua, lakini upendo huimarisha uhusiano na kuufanya uendelee.

Kupotea kwa mihemko kwa kawaida ni kwa sababu ya majukumu mengine ambayo huuchukua muda wa mapenzi au hubadili mwonekano wa mpenzi wako. Haya yote yanaweza kuondolewa kwa kuwa na muda wa kimapenzi pamoja. Kitu ulichokipenda mwanzoni mwa uhusiano kwa mpenzi wako kinapaswa kuendelea katika kipindi chote cha uhusiano. Uhusiano ni kutumia muda mkiwa pamoja. Uhusiano mwingi huisha kwa sababu ya kukosekanakwa tabia hii.

Iwapo watu wataingia kwenye mapenzi kwa sababu sahihi na kuwa na udhati moyoni na mapenzi hayo na kujenga uhusiano wao na kuendelea kutumia muda pamoja na kusaidiana, uhusiano huo wa kimapenzi utadumu kwa muda mrefu zaidi.

Watu wana malezi tofauti na hivyo kuwa na malengo na matarajio tofauti. Hii ndiyo sababu pindi wanapokutana na mtu mpya kwa mara ya kwanza, wanataka kumjua na kuona kama wako katika ngazi moja. Vitu vingi zaidi vya pamoja unavyoweza kuwa na mtu hufanya uhusiano mzuri zaidi. Mawasiliano ni msingi wa uhusiano wowote. Wenza wanaozungumza hudumu kwenye mapenzi na wenza wasiozungumza huachana. Hivyo, unapokutana na watu wapya unapaswa kuwajua kwanza. Kabla ya kukutanisha viungo vya uzazi, kuwe na kukatana kwa fikra.

Uhusiano unaofanikiwa hujijenga kwenye imani, uaminifu, upendo, uvumilivu, kufanya mambo pamoja na kusameheana.

Uhusiano mwingi unaovunjika hukosa moja au zaidi ya vitu hivi.
 

 






No comments:

Post a Comment