“When men and women are able to accept and respect their differences then love has a chance to blossom.”
Monday, January 5, 2015
perfecting love making..
Wapendwa wasomaji wa Blog yetu,
Leo ningependelea walau kidogo kuigusa ile issue nyeti ambayo inawahusu wadau wangu wote wa blog-nikimaanisha VIJANA, WENYE MAHUSIANO na WALE walio katika NDOA. Lakini nitaizungumzia kwa kifupi nikigusia vipengele muhimu kwa matumaini kwamba itasaidia wale wote ambao wataizingatia na kuifanyia kazi. Mtaniwia radhi kwani nitazungumzia from men's perspective zaidi kidoogo kwa leo.
Tendo la kufanya mapenzi na mwanamke ni kipaji ambacho kila mwanaume rijali anadhani anacho. Lakini ki ukweli wapo wanawake wengi ambao wanaachwa wakiwa hawajaridhika mara baada ya kufanya mapenzi na wapenzi wao!
Bahati mbaya sana mara nyingi wanaume hawa wamekuwa wakipata ushauri toka kwa marafiki, kwa stori za vijiweni ama mtaani na wengine toka katika picha za ngono! Na kwana namna hiyo wamekuwa na dhana potofu kuhusu maana halisi ya kufanya mapenzi!
Wataalamu wa mambo ya mapenzi na mahusiano wanasema kwamba unapotaka kufanya mapenzi lazima ufuate utaratibu unaokubalika ambao umehakikiwa kumridhisha mwanamke baada ya tendo lenyewe.
*Utaratibu huu huwa una vipengele vitano (get her to the mood, practice fore play, Oral sex, Teasing and the act itself). Kwangu mimi pamoja na vipengele hivyo muhimu ningependa kuongelea mambo muhimu na ya msingi ambayo huboresha tendo hilo: (mwishoni kukiwa na dodoso kwa wasiozingatia..)
1. Maelewano- ili kuweza kufanya mapenzi na kila mmoja wenu akaridhika bila tatizo ni muhimu sana mkawa na freedom of mind and souls, kama wapenzi mkiwa katika migogoro na ugomvi mazingira ya kuwavutia kufanya ama ku enjoy tendo la ndoa hayatakuwepo, hivyo ni muhimu kuwa katika maelewano mazuri kabla ya kutaka kufanya mapenzi. (Watu wengi wamechukulia kama kufanya mapenzi baada ya ugomvi ama kutokuelewana ndiyo suluhisho la kumaliza ugomvi, hiyo ni kasumba na tatizo kwani mnafuga ugonjwa ambao utakuja kuwa tatizo kubwa mbeleni..zungumzeni na kumaliza tofauti zenu kabla. Kinyume na hapo ni kuudhalilisha tu utu wako.)
2. Usafi - Usafi ni muhimu sana kwa mwanaume lakini pia na hasa kwa mwanamke, hapa naongelea usafi wa mwili, kila mtu anafahamu umuhimu wa kuweka mwili safi kabla, baada ya kushiriki tendo ambalo linahusu kuukabidhi mwili wako kwa mwenzi wako kwa muda husika. Usafi wa mwili huongeza pia mvuto na kutoa uhuru zaidi kwa mwenzako ku enjoy kufanya mapenzi na wewe na ushirikiano muafaka! Mbali na usafi wa mwili ni muhimu pia kuzingatia usafi wa mazingira mnayofanyia tendo hilo, kwani mta relax na ku enjoy zaidi mazingira yakiwa safi na ni salama kwa afya ya mwili pia. (Washikaji wengine unakuta kwapa ama kinywa kinatema lakini ndiyo kwanza anataka game na ufundi kibao! Unaweza ukaenda ktk faragha nyingine, kwa mfano hotelini, unakuta mazingira ya sehemu ni ya kutumika na nyie kwa uchu mnajiachia tu! Jali afya yako..pangilia, vuta subira, tengeneza mazingira, safisha kiwanja, hata kama mnaamua kujiachia bafuni basi kuwe kusafi!)
3. Utayari- ni muhimu kusiwepo na mazingira ya kulazimishana kufanya mapenzi, kila mmoja awe ameridhia tendo hilo, mfano kutembea na mpenzi wa mtu, mtoto wa chini ya umri ama mwanafunzi au mume ama mke wa mtu, kufanya mapenzi kwa uhuru na mpenzi wako kuna nafasi nzuri zaidi kufurahia tendo la ndoa, lakini pia kumbuka kuna madhara ya kisaikolojia ambayo unaweza kuyapata bila kujua mara baada ya kufanya tendo hilo kwa kulazimishana au na mpenzi ama mume/mke wa mtu. (Uko usemi wa sisi waswahili kwamba cha mtu kitamu lakini huo ni ulimbukeni tu kwani kumbuka unajenga mazingira hatarishi na si salama kwa kuendekeza ngono zembe. Pia mla cha mwenzie... lakini kuna magonjwa na kufumaniwa pia.. usijenge aibu ama uadui katika maisha sababu ya tamaa ya muda mfupi, kufanya ngono tu!)
Ni vizuri pia mkawa mmekula vizuri, kuna vyakula ambavyo ni vyepesi ambavyo pia havi-keri kwa harufu ama uchovu wa kuvimbiwa, vivyo hivyo kuna vinywaji na matunda ambayo yanaendana na shughuli hii pevu bila ya kuzidisha kiwango! Muwe sehemu ambayo ni ya faragha, salama na inayokubalika walau, mapenzi yana sehemu zake huwezi fanya popote tu pale, faragha uleta uhuru zaidi.(Jamaa wengine wanatwanga mzee wa meza kama kilo na bia kadhaa, makachumbali kibao yenye vitunguu swaumu, fegi kwa wingi matokeo yake ni kukerana tu kitandani pamoja na kutoa hewa chafu! Jamaa wengine nao tena waume ama wake za watu bila aibu wanamalizaga haja zao katika vyoo vya bar na guest bubu za vichochoroni-lindeni utu na heshima zenu. Utu hauna thamani/haununuliki!)
4. Relaxation - hakuna kitu kingine muhimu kama kuuweka mwili katika mazingira ya kurelax, ondokana na mawazo na stress na focus katika shughuli iliyo mbele yako, utafanikiwa ku enjoy sana unapofanya mapenzi na mwenzi wako. Usisahau umuhimu wa kushirikishana mara baada ya kuanza kushiriki tendo lenyewe, hamna budi ku enjoy each and every moment ya game. *Mnaweza sasa kupitia hatua tano za wataalamu nilizotangulia kuzitaja awali hapo juu. (Jamaa wengine utakuta anaingia kwenye game, kipenga kimelia tu yeye na goli hajali kuna mabeki kati nyuma wala nini, piga, kamua, piga.. duh! ni kweli wako wanaoridhishwa na game kama hizo lakini jaribu tofauti kidogo wakati mwingine uone matokeo, wako wenzetu pia wengine game imeanza lakini wao na sms, mara simu mara gazeti, jamani hizi shughuli huwa zina unyeti wake na kustahili kupewa wasaa, siyo wakati wa kuboana!.)
6. Jambo la mwisho na la muhimu kwangu la kuzingatia ni Usalama - Siyo jambo jema kufanya tendo la ndoa kama mmojawapo ana magonjwa ya kuambukia ya aina yoyote, labda kama mtakubaliana na kuchukua tahadhari stahili, muwe makini kuzuia mimba zisizotarajiwa ama kwa kutumia kinga ama njia yeyote mliyokubaliana ambayo haitamkwaza yeyote kati yenu, pia kuna magonjwa sugu na hatarishi kama STDs na Ukimwi-ni vyema kuchukua tahadhari kutomwamini na kufanya mapenzi na mtu ambaye hujui status yake kiafya! (Magonjwa kama Ukimwi hauonekani kwa macho na unampata yeyote, wakati wowote, na tuzingatie kwamba wako binadamu wengine wasio na utu wanaosambaza ugonjwa wa Ukimwi kwa makusudi! Ni jambo la kusikitisha endapo starehe na furaha ya muda mfupi itakuja geuka kuwa sononeko la maisha yako yote!)
Kwa leo wapendwa wa blog naishia hapa, lengo la makala hii ni kutaka kusadia kuboresha namna ambavyo mnaridhishana katika kufanya mapenzi lakini wakati huo huo kukufanya uweze kuchukua tahadhari kwa yote yanayoweza kujitokeza katika mazingira tofauti.
Mbarikiwe katika mahusiano yenu!
Labels:
MARRIAGE,
RELATIONSHIP
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment